Wednesday, August 8, 2012


                
              SEMA NA MAZINGIRA YAKO

KAMA UNA MAKARA INAYOHUSU MAZINGIRA NA AFYA YA JAMII KWA UJUMLA, TUMA KWA EMAIL IFUATAYO- envirofamilytz@gmail.com UTAPATA FULSA YA MAKALA YAKO KURUSHWA KATIKA BLOG HII INAYOHUSU JAMII NA MAZINGIRA YAKE. KWA KUPITIA BLOG HII, KWA PAMOJA TUNAWEZA KUIFANYA JAMII KUWA NA MTAZAMO SAHII JUU YA MAZINGIRA SAFI NA SALAMA.

  1. FUATA HATUA ZIFUATAZO KWENYE KUTUMA.
  • Andika makala yako kwa makini na lugha sahii
  • Pitia makala yako kwa uangalifu
  • Tuma ujumbe mfupi kwa kutumia Email adress yetu tuliyokupa hapo juu kisha andika jina lako namba ya simu pamoja na eneo unalokaa.
  • Tuma makala yako kwa Email address uliyopatiwa hapo juu.

                                           Imeandaliwa na Phillip Wangwe. 2012.


 

GIVE THE WAY WATER TO PASS-YAPE MAJI NJIA YA KUPITA.

Miongoni mwa vitu vinavyo changia uaribifu wa vyanzo vya maji ni pale wanajamii wanapo haribu uasilia wa vyanzo hivyo. Envirofamily Tanzania inawaomba wanajamii kuwa waangalifu dhidi ya huaribifu wa vyanzo hivyo. Mabadiliko ya Tabia Nchi ni miongoni mwa tatizo kubwa linalotawala nyanzo zote katika maisha. Tuwe marafiki na mazingira yetu ili tufanikishe malengo yetu. Envirofamily kupitia Blog hii itatoa mitazamo mbali mbali ikiwemo elimu kwa Jamii husika juu ya swala hili la muhimu katika Dunia yetu.Kutakuwa na mfululizo wa makala kwa muda wa mwezi mmoja, hivyo ndugu waosaji na wafuatiliaji wa blog hii fuatilia mara kwa mara na tunaitaji maoni yako juu ya swala hili. Envirofamily imelenga kushirikisha mawazo ya wanajamii katika kutatua maswala mbalimbali. (Wangwe P. 2012).

Envirofamily Tanzania (2012).

     MAJI NI UHAI, TUTUNZE VYANZO VYA MAJI. KWA FAIDA YA SASA NA MAISHA YA BAADAYE.

Ndugu Mtanzania, Jukumu sio la serikari peke yake, bali sote tunahusika. Hakikisha unatunza vyanzo vya maji kwa kutokata miti ovyo, kutochoma moto na kilimo kisicho sahii.Mabadiliko ya tabia Nchi yanapelekea kuwepo kwa matatizo mbalimbali yanayo athiri maisha yetu na viumbe hai vingine hapa duniani.

Mtanzania amka uyapende mazingira yako kwa faida yetu sote.