ENVIROFAMILY TANZANIA.
Mwanzilishi wa jumuhia hisiyo ya Kiserikari bwana Phillip Wangwe amewaomba wadau mbali mbali wa mazingira kuwa kipao cha mbele katika kujitolea katika maswala mbali mbali ya utunzaji wa mazingira hapa nchini. Hakiongea na wananchi wa eneo la Mbezi beach Hivi karibuni, aliwaomba wadau na wananchi kujitolea kwa hali na mali kulinda na kutunza mazingira. Hatuna haja ya kusubiri wadhamini ilituweze kufanya shughuri hizi za mazingira'Akisema Bwana Phillip Wangwe.
Utamaduni wa kujitolea ni miongoni mwa hatua kubwa iliyofikiwa na Nchi mbali mbali zilizoendelea. Hivi karibuni Mwanzilishi wa Asasi hii Bwana Phillip Wangwe alikuwepo Nchini Norway Kimasomo ndiko alipoona jinsi gani watu wanavyo heshima taratibu zao katika maisha yao ya kila siku. Moja ya jambo muhimu katika maisha ni Mazingira bora na salama. Hakiongea na wadau mbali mbali hizi karibuni alisema''Ni lazima tuwe na mwamko uliyopitiliza kwani hali ya Nchi yetu hizi sasa ni mbaya hasa katika maeneo ya mijini kwani kunajumla ya matatizo mengi yanayoitaji ufumbuzi yakunifu. Moja ya matatizo makubwa ni afya ya wakazi wengi ambalo linatokana na uchafuzi mkubwa katika maeneo ya makazi na biashara.
Tukipenda mazingira, nayo yatatupenda kwani mazingira ni sehemu ya familia zetu, Hivyo ni lazima kila mmoja wetu awe karibu na swala zima la utunzaji wa mazingira.(Phillip w. 2012)